09. Hadiyth “Kila kitendo kina shauku na kila shauku ina muda wake… “

57- Ibn Hibbaan vilevile ameipokea katika “as-Swahiyh” yake kupitia kwa Abu Hurayrah ambaye ameeleza kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Kila kitendo kina shauku na kila shauku ina muda wake. Ikiwa mwenye nayo ni mwenye kufanya vizuri na kati kwa kati, basi wekeni matarajio kwake. Na kama ananyooshewa vidole, basi msimuhesabu.”[1]

Shauku ya vijana ni mwanzo na mwisho wao.

[1] Swahiyh.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Adhwiym bin ´Abdil-Qawiy al-Mundhiriy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb (1/131)
  • Imechapishwa: 27/04/2020
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy