09. Hadiyth ”Hakuna hasadi isipokuwa katika mambo mawili… “

75- Ibn Mas´uud amesimulia kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Hakuna hasadi isipokuwa katika mambo mawili: mtu ambaye Allaah amempa mali na akawa anaitumia kwa haki na mtu ambaye Allaah amempa hekima na akawa anahukumu kwayo na anaifunza.”

Ameipokea al-Bukhaariy na Muslim.

Kunaposemwa hasadi kunamaanishwa mtu akatamani neema ilio kwa yule anayemuhusudu imwondoke. Jambo hili ni haramu. Hasadi inaweza pia kuwa na maana mtu akatamani kuwa na kile alichonacho mwenzake. Jambo hili halina neno na ndio kilichokusudiwa hapa.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Adhwiym bin ´Abdil-Qawiy al-Mundhiriy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb (1/141)
  • Imechapishwa: 15/09/2018
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy