09. Du´aa wakati wa kutoka nyumbani


44- Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Yule mwenye kusema wakati anapotoka nyumbani:

بِسْمِ اللهِ تَوَكَّلْتُ عَلى اللهِ وَلاَ حَوْلَ وَلاَ قُوَّةَ إِلاَّ باللهِ تَعَالى

“Kwa jina la Allaah. Ninamtegemea Allaah. Hapana mabadiliko wala uwezo isipokuwa kwa msaada wa Allaah (Ta´ala) mwambie: “Umekingwa, umelindwa na kuongozwa.” Ataokolewa na Shaytwaan na kumwambia Shaytwaan mwengine: “Utamfanya nini mtu ambaye ameongozwa, amekingwa na amelindwa?”

45- Ummu Salamah (Radhiya Allaahu ´anha) amesema:

Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hajawahi kutoka nyumbani isipokuwa alikuwa anaangalia juu mbinguni na kusema:

اللَّهُمَّ إِنِّي أَعُوذُ بِكَ أَنْ أَضِلَّ أَوْ أُضَلَّ أَو أَزِلَّ أَوْ أُزَلَّ أَوْ أَظْلِمَ أَو أُظْلَمَ أَوْ أَجْهَلَ أَوْ يُجْهَلَ عَليَّ

“Ee Allaah! Najikinga Kwako kutokana na kupotea au kupoteza, kuteleza au kumtelezesha mtu, kudhulumu au kudhulumiwa, kuwa mjinga au kufanywa mjinga.”

  • Mhusika: Shaykh-ul-Islaam Ahmad bin Taymiyyah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ul-Kalim at-Twayyib, uk. 44-45
  • Imechapishwa: 21/03/2017