09. Da´wah ya Mtume kwa watoto


Aayah hizi zinafahamisha kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alitumwa ili awaamrishe watu kumuabudu Allaah peke yake na kuwakataza kumuabudu mwengine asiyekuwa Allaah. Hii ndio dini yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ambayo aliwalingania watu kwayo na akawapiga vita kwayo. Allaah (Ta´ala) amesema:

وَقَاتِلُوهُمْ حَتَّىٰ لَا تَكُونَ فِتْنَةٌ وَيَكُونَ الدِّينُ كُلُّهُ لِلَّـهِ

“Na piganeni nao mpaka kusiweko fitnah na Dini yote iwe kwa ajili ya Allaah.”[1]

Fitnah ni shirki.

Allaah (Ta´ala) alimtuma Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alipokuwa na miaka arubaini. Miaka kumi aliwalingania watu katika kumuabudu Allaah peke yake na kuacha kumuabudu mwengine asiyekuwa Allaah. Baada ya hapo akasafirishwa kupandishwa mbinguni. Huko juu akafaradhishiwa kuswali swalah tano. Pindi Allaah (Ta´ala) alipomfaradhishia (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hapakuwepo mkati kati yeyote baina yake na Allaah.

Baada ya hapo akaamrishwa kuhajiri. Akahajiri kwenda al-Madiynah. Vilevile akaamrishwa kutoka kwenda katika Jihaad. Karibu miaka kumi akatoka kwenda kupigana Jihaad kwa ajili ya Allaah mpaka watu wakasilimu kuingia katika dini ya Allaah makundi kwa makundi.

Wakati Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alipofikisha miaka sitini na tatu na Allaah (Ta´ala) akaikamilisha dini kupitia kwake na akamfanya kufikisha ujumbe wa Allaah, ndipo akafariki. Swalah na salaam ziwe juu yake.

[1] 08:39

  • Mhusika: Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ta´liym-us-Swibyaan at-Tawhiyd, uk. 27-29
  • Imechapishwa: 25/03/2017