09. Dalili ya saba kutoka katika Sunnah kwamba Allaah yuko juu ya viumbe


7- Abu Muhammad bin ´Abdillaah bin Mansuur al-Mawsiliy ametukhabarisha: Abul-Husayn bin at-Twuyuur ametuhadithia: Muhammad bin ´Abdil-Waahid bin Ja´far ametuhadithia: Ahmad bin Ibraahiym bin Shaadhaan ametuhadithia: Ahmad bin Muhammad bin al-Mughallas ametuhadithia: Sa´iyd bin Yahyaa al-Umawiy ametuhadithia: ´Abdullaah bin Ziyaad ametuhadithia, kutoka kwa Ibn Ishaaq: Yaziyd bin Sinaan amenihadithia, kutoka kwa Sa´iyd bin al-Ujayrid al-Kindiy, kutoka kwa al-´Irs bin Qays al-Kindiy, kutoka kwa ´Adiy bin ´Umayrah bin Farwah al-´Abdiy aliyesema:

“Karibu na sisi tulikuwa myahudi aliyekuwa akiitwa Ibn Shalaa. Siku moja nikakutana naye ambapo akasema: “Mimi nimesoma katika Kitabu cha Allaah kilichoteremshwa kwamba watu wa Peponi wanamuabudu Allaah juu ya nyuso zao. Ninaapa kwa Allaah kwamba sijui sifa hii kwa watu wengine zaidi ya sisi mayahudi. Nimesoma pia kuwa Mtume wao atakuwa ni mwenye kutoka Yemen. Yule mwenye kumfuata atakuwa katika uongofu. Hatuoni kuwa anatoka kwengine isipokuwa kwetu sisi mayahudi. Nimesoma pia kuwa kutatokea ajali mbili, moja itakuwepo Misri na nyingine Swiffiyn.” Ninaapa kwa Allaah kwamba haikuchukua muda mrefu mpaka tukafikiwa na khabari kwamba kuna mtu kutoka katika ukoo wa Haashim amekuwa Mtume na anasujudu juu ya uso wake. Nikakumbuka maneno ya bn Shahlaa na nikahajiri kwenda kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Ndipo nikamuona yeye na Maswahabah wake wanasujudu juu ya nyuso zao na wanasema kuwa Mola wao yuko juu ya mbingu, ambapo nikasilimu na kumfuata.”[1]

[1] al-Iswaabah (4/447) ya Ibn Hajar na al-´Uluww, uk. 25, ya adh-Dhahabiy aliyesema:

“Hadiyth ni geni.”

  • Mhusika: Imaam Muwaffaq-ud-Diyn bin Qudaamah al-Maqdisiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ithbaatu Swifat-il-´Uluww, uk. 78-79
  • Imechapishwa: 16/04/2018