09. Baada ya ubainifu huu kuna yeyote mwenye kutilia mashaka ´Aqiydah ya Shaykh?


Allaah ameitakasa nafsi Yake kutokamana na yale wanayomsifia kwayo wakhalifu miongoni mwa Ahl-ut-Takyiyf na Ahl-ut-Tamthiyl na kutokamana waliyomkanushia kwayo wakanushaji miongoni mwa upotoshaji na ukanushaji. Amesema:

سُبْحَانَ رَبِّكَ رَبِّ الْعِزَّةِ عَمَّا يَصِفُونَ وَسَلَامٌ عَلَى الْمُرْسَلِينَ وَالْحَمْدُ لِلَّـهِ رَبِّ الْعَالَمِينَ

”Utakasifu ni wa Mola wako,  Mola mtukufu kutokana na yale wanayoyasifu na mmani iwe juu ya Mitume na himdi zote nejma anastahiki Allaah, Mola wa walimwengu.”[1]

Ameitakasa nafsi Yake (Subhaanahu wa Ta´ala) kutokamana na madhehebu ya mapote mawili – madhehebu ya Mumaththilah na madhehebu ya Mu´attwilah – na akajithibitishia majina na sifa kwa njia inayolingana na utukufu Wake (Subhaanahu wa Ta´ala). Kwa ajili hiyo akasema:

سُبْحَانَ رَبِّكَ رَبِّ الْعِزَّةِ عَمَّا يَصِفُونَ

”Utakasifu ni wa Mola wako,  Mola mtukufu kutokana na yale wanayoyasifu.”

Akasema vilevile:

سُبْحَانَ اللَّـهِ عَمَّا يُشْرِكُونَ

“Utakasifu ni wa Allaah kutokana na yale wanafanya shirki.”[2]

Ameitakasa nafsi Yake kutokamana na hayo. Haya ndio madhehebu ya haki na ndio wanayofuata Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah. Ndio ambayo anaamini Shaykh (Rahimahu Allaah) na akasema:

“Ndio ´Aqiydah na yale anayoamini.”

Amesema (Ta´ala):

سُبْحَانَ رَبِّكَ رَبِّ الْعِزَّةِ عَمَّا يَصِفُونَ

”Utakasifu ni wa Mola wako,  Mola mtukufu kutokana na yale wanayoyasifu.”

Ameitakasa nafsi Yake kutokamana na yale wanayomsifia Ahl-ut-Ta´twiyl na Ahl-ut-Tamthiyl. Kisha akasema:

وَسَلَامٌ عَلَى الْمُرْسَلِينَ

“Amani iwe juu ya Mitume.”

Amewasalimia kutokana na usalama wa yale waliyoyasema juu ya Allaah (´Azza wa Jall) kumsalimisha kutokamana na kasoro na mapungufu. Mitume wamemsifia Allaah kwa yale aliyojisifia nafsi Yake. Kwa ajili hiyo ndio maana Allaah akawasalimia na akamalizia Aayah kwa kusema:

وَالْحَمْدُ لِلَّـهِ رَبِّ الْعَالَمِينَ

“Himidi zote njema anastahiki Allaah, Mola wa walimwengu.”[3]

Yeye ndiye Mwenye sifa na himdi zote. Hakuna mwengine anayestahiki hayo isipokuwa Yeye (Subhaanahu wa Ta´ala). Je, baada ya ubainifu huu kuna yeyote anayefikiria kuwa Shaykh ana kitu anachokwenda kinyume na wanachuoni kama wanavyomtuhumu wapinzani wake? Hapana. Hii ndio ´Aqiydah yake ilio wazi na safi kabisa kutokamana na yale wanayomtuhumu kwayo katika shububa mbalimbali.

[1] 37:180-182

[2] 52:43

[3] 37:180-182

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Aqiydat-il-Imaam Mujaddid Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab, uk. 27
  • Imechapishwa: 03/03/2021