09. Allaah anapotosha kwa uadilifu

… na akampotosha ambaye amemtosa kutokana na hekima Yake – Allaah anamuwafikisha na kumtukuza yule mwenye kukubaki na kutaka haki. Pia Allaah anampoteza yule mwenye kuipa mgongo haki na haikubali hali ya kuwa ni malipo kwake. Kwa hivyo anamwongoza amkaye kwa fadhilah Zake na anampotosha amtakaye kwa uadilifu Wake. Ambaye haikubali haki basi Allaah (´Azza wa Jall) anamkosesha nayo. Huo ni uadilifu wa Allaah na sio dhuluma. Kwa sababu yeye ndiye ambaye hakuikubali haki, haitaki haki na anafanya kiburi kwa viumbe. Hivyo basi Allaah hamwongozi uongofu wa kuafikishwa. Hayo ndio malipo na adhabu yake. Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) hakumdhulumu. Allaah (Ta´ala) amesema:

فَلَمَّا زَاغُوا أَزَاغَ اللَّـهُ قُلُوبَهُمْ

“Basi walipopotoka, basi Allaah akapotosha nyoyo zao.”[1]

وَنُقَلِّبُ أَفْئِدَتَهُمْ وَأَبْصَارَهُمْ كَمَا لَمْ يُؤْمِنُوا بِهِ أَوَّلَ مَرَّةٍ وَنَذَرُهُمْ فِي طُغْيَانِهِمْ يَعْمَهُونَ

“Tunazigeuza nyoyo zao na macho yao kama wasivyoiamini mara ya kwanza na tunawaacha katika upetukaji wao wakitangatanga.”[2]

Pindi mtu haikubali haki basi Allaah anamjaribu kwa batili na upotevu.

[1] 61:5

[2] 6:110

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Bayaan-ul-Ma´aaniy fiy Sharh Muqaddimati Ibn Abiy Zayd al-Qayrawaaniy, uk. 15-16
  • Imechapishwa: 01/07/2021