Hizi ndio sampuli tatu za Tawhiyd:

1- Tawhiyd-ur-Rubuubiyyah. Aina hii mara nyingi hakuna yeyote mwenye kuipinga.

2- Tawhiyd-ul-Uluuhiyyah. Aina hii wengi wanaipinga na hakuna wenye kuithibitisha isipokuwa tu wafuasi wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Amesema (Ta´ala):

وَإِن تُطِعْ أَكْثَرَ مَن فِي الْأَرْضِ يُضِلُّوكَ عَن سَبِيلِ اللَّـهِ

“Ukiwatii wengi walioko ulimwenguni, basi watakupoteza kutokamana na njia ya Allaah.”[1]

وَمَا يُؤْمِنُ أَكْثَرُهُم بِاللَّـهِ إِلَّا وَهُم مُّشْرِكُونَ

”Wengi kati yao hawamwamini Allaah isipokuwa wao ni wenye kufanya shirki.”[2]

Hakuna walioithibitisha Tawhiyd-ul-Uluuhiyyah isipokuwa tu wafuasi wa Mitume. Ni waumini wa kila nyumati. Wameithibitisha Tawhiyd-ul-Uluuhiyyah na washirikina wa kila zama na mahali wakaipinga.

3- Tawhiyd-ul-Asmaa´ was-Swifaat. Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah wanathibitisha majina na sifa za Allaah. Sambamba na hilo Jahmiyyah, Mu´tazilah, Ashaa´irah na vifaranga vyao wanaikengeusha na kuzipindisha maana. Baadhi yao wamezikanusha zote kwa ujumla na wengine baadhi yake. Muhimu ni kujua namna wanavyoamini Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah katika jambo hili.

[1] 06:116

[2] 12:106

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: I´aanat-ul-Mustafiyd bi Sharh Kitaab-it-Tawhiyd, uk. 25
  • Imechapishwa: 23/07/2019