Allaah (Jalla wa ´Alaa) amesema:

هُوَ الَّذِي أَرْسَلَ رَسُولَهُ بِالْهُدَى وَدِينِ الْحَقِّ

“Yeye Ndiye aliyemtuma Mtume Wake kwa uongofu na dini ya haki.” (09:33)

Uongofu ni elimu yenye manufaa. Dini ya haki ni matendo mema. Lazima mtu akusanye mambo mawili; elimu yenye manufaa na matendo mema. Hayo ndio aliokuja nayo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Hakuja na elimu bila ya matendo kama ambavyo vilevile hakuja na matendo tu bila ya elimu. Ni mambo mawili yanayoenda sambamba.

Ni lazima matendo yajengwe juu ya elimu na ujuzi. Ni lazima kwa msomi atendee kazi elimu yake. Vinginevyo msomi asiyeifanyia kazi elimu yake na mtendaji asiyetenda juu ya elimu, wote wawili ni waangamivu. Isipokuwa tu yule ambaye yuko na elimu yenye manufaa na matendo mema. Allaah amemtuma Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwa mambo haya.

  • Mfasiri: Firqatunnajia.com