08. Watoto wa waislamu wanatakiwa ku§itwa namna hii

Utoaji wa jina kumpa mtoto ni jambo sahali na lepesi na himdi zote zinamstahikia Allaah. Ni jambo lisilohitajia utafiti wala kamusi. Utoaji jina kumpa mtoto ni jambo linahusiana tu na kukutana na maana ya Shari´ah na usalama wa kimaumbile. Waislamu wanatakiwa kuhakikisha wamempa mtoto wao mchanga aliyezaliwa:

1- Jina lenye kuthibitisha kuwa ni mja wa Allaah (Ta´ala)

2- Majina ya waja wema Manabii na Mitume wa Allaah.

3- Majina ya Maswahabah wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

4- Majina ya waliokuja baada yao waliowaiga.

5- Majina mengineyo ya kiarabu.

Muislamu achague jina lisilokataliwa na Shari´ah. Na ikiwa ameshindwa kujiamulia jina basi na aende kwa mwanachuoni ambaye anajulikana kwa maoni mazuri, ´Aqiydah safi na ladha iliosalimika amtake ushauri. Maswahabah walikuwa wakiwapeleka watoto wao wachanga wenye kuzaliwa kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ili awape majina. Hii ni dalili yenye kuonesha kuwa ni jambo limewekwa katika Shari´ah kuwataka ushauri wanachuoni na wanafunzi.

  • Mhusika: ´Allaamah Bakr bin ´Abdillaah Abu Zayd
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Tasmiyat-ul-Mawluwd, uk. 08
  • Imechapishwa: 18/03/2017