08. Wanazuoni wengine kuhusu sherehe ya usiku wa nusu ya Sha´baan


Haafidhw al-´Iraaqiy amesema:

“Hadiyth kuhusu usiku wa nusu [ya Sha´baan] ametungiwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na ni amesemea uongo.”

Imaam an-Nawawiy amesema katika kitabu “al-Majmuu´”:

“Swalah inayotambulika kama ´Swalaat-ur-Raghaaib` ambayo ni Rak´ah kumi na mbili kati ya Maghrib na ´Ishaa usiku wa ijumaa ya kwanza ya Rajab na swalah ya usiku wa nusu ya Sha´baan Rak´ah mia moja, swalah mbili hizi ni Bid´ah mbili zilizokemewa. Msidanganyike na kutajwa kwake ndani ya kitabu “Quut-ul-Quluub”, “al-Ihyaa´ ´Uluum-id-Diyn” wala Hadiyth zinazozizungumzia swalah mbili hizo. Yote hayo ni batili. Wala msidanganyike na baadhi ya wale maimamu ambao wametatizika na kuzihukumu ambapo wakatunga tungo juu ya kupendekeza kwazo. Hakika wamekosea katika jambo hilo.

Shaykh na Imaam Abu Muhammad ´Abdir-Rahmaan bin Ismaa´iyl kitabu chenye thamani juu ya kuzibatilisha. Amefanya vyema na vizuri. Wanazuoni wana maneno mengi juu ya suala hili. Endapo tutanakili kila maneno tuliyoyaona juu ya jambo hili basi maneno yangerefuka. Pengine katika tuliyoyataja kunatosheleza na kunamkinaisha kwa yule ambaye anaitafuta haki.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Tahdhiyr minal-Bid´ah, uk. 29-30
  • Imechapishwa: 18/01/2022