08. Ushabiki wa wakristo na chuki zao dhidi ya Uislamu

Niliposoma kwenye gazeti al-Miythaaq basi nikakumbuka ushabiki wa wakristo, jeuri yao na mtazamo wao juu ya Uislamu kwa jichi la makengeza. Yalinikumbusha tukio lililonikumba.

Pindi nilipokuwa India nikifanya kazi ya uprofesa kwenye chuo kikuu Nadwat-ul-´Ulamaa´ kwa mwaliko wa Sulaymaan an-Nadwiy na Dr. ´Abdul-´Aliyy. Nikaona kuwa ni lazima nijue lugha ya kigeni. Leo hii haiwezekani kupata elimu kwa njia nyingine. Lugha yenye kuongoza India ni kingereza na kwa ajili hiyo nikaanza kujifunza kingereza kwa wanafunzi wangu na wengineo. Tokea hapo mwanzo nikaona kuwa kingereza cha wahindi hakiafikiani na utamshi wa wangereza na ufaswaha wao. Hivyo nikaenda kwenye shule ya kimisionari ya mkristo mmoja iliokuwa ikiongozwa na mtu wa Canada. Nikamuomba anifunze kingereza na nitamlipa. Akanambia kuwa yeye hapokei malipo na kwamba nitapiga hatua kubwa endapo nitafuatilia darasa zake kwenye shule ya kimisionari. Nikamwambia kuwa mimi bado ndo naanza na kwamba sintoelewa darasa. Akanambia nihudhurie na kwamba kwa wiki atanipa darasa tatu na kila darasa moja itakuwa ni dakika 30.

Nikaanza kwenda kwenye darasa. Alikuwa ameshakuwa mtumzima amefikisha miaka 50. Alikuwa hana uchangamfu na shauku ya kazi yake. Alikuwa akihubiria tu ili aweze kupata kueshi. Hakuna walioitikia wito wake isipokuwa tu wachache. Watu wachache tu ndio walikuwa wakihudhuria darasa zake. Watu watatu tu ndio walikuwa wakihudhuria darasa zake. Pamoja na mke wake ndio wanakuwa wanne na mimi ndio tunakuwa watano.

Ilipokaribia kufika Krismasi kukafanywa matangazo kwenye magazeti ya kwamba kutapitishwa kisa cha maisha ya ´Iysaa. Wakadhuhuria wasikiliza wengi mpaka shule ya kimisionari ikajaa. Akamwita padiri mwingine aje kumsaidia kuhubiria. Walikuwa wakisaidiana kuhubiri na kuelezea sura mpaka sherehe ikaisha. Ndipo akanivamia yule padiri mwingine. Alikuwa ni kijana kutoka Marekani na alikuwa akiitwa Smith. Ilikuwa mwaka wa 1349, sawa na 1930.

  • Mhusika: ´Allaamah Muhammad Taqiyy-ud-Diyn al-Hilaaliy al-Maghribiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Baraahiyn al-Injiylyyah ´alaa anna ´Iysaa daakhil fiyl-´Ubuudiyyah wa la hadhdhwa lahu fiyl-Uluuhiyyah, uk. 24-25
  • Imechapishwa: 16/10/2016