08. Uchochezi wa Raafidhwah Makkah ni mfano wa ugaidi

7- Mapigano ya kishaytwaan na ya kigaidi yaliyofanywa na Raafidwah waabudu moto na wafuasi wa serikali ya Khomeini ya Iraan katika mnasaba wa hajj siku ya ijumaa tarehe 06 Dhul-Hijjah mwaka 1407 ni mfano mwingine tena wa ugaidi wa kidhambi na wenye kukemewa.

Ajali yenyewe kubwa ilikuwa pindi wafuasi wa Khomeini walipofanya maandamano makubwa ya fujo nje ya msikiti Mtakatifu. Wakaeneza vipeperushi vilivyokuwa na uchochezi na fitina. Malengo yao ilikuwa kuwashtua watu wenye amani na kuibadilisha hajj nzuri kwenda katika sehemu ya ghasia na fujo na matokeo mabaya. Walianza kuvunja milango ya maduka na magari na wakayawashia moto na wale wamiliki wa magari. Ufisadi huu mkubwa ulisababisha khasara kubwa. Mali nyingi ziliharibika, watu wengi walikufa. Siku hiyo watu mia nne na mbili walipoteza uhai ambapo thamanini na tano walikuwa ni watu wenye kuchunga amani na raia wa kisaudia. Baadhi wakaanza kuandamana ili kusababisha vita ugomvi kati ya waislamu na kuwafanya wakagombana na kuutweza msikiti Mtakatifu. Zikawahakikia ghadhabu za Allaah na wakapatwa na kuteremkiwa na hasira Zake na wakapigwa na dhoruba kubwa na likawasambaratisha kabisa kabisa. Laana za Allaah zimwandame kila mwongo mtenda dhambi, dhalimu na mkemewaji aliyepindukia.

  • Mhusika: ´Allaamah Zayd bin Muhammad al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Irhaab, uk. 16-17
  • Imechapishwa: 03/04/2017