08. Qur-aan yote ni Tawhiyd


Qur-aan tukufu yote inazungumzia Tawhiyd:

1- Inaamrisha kumwabudu Allaah pekee na kutomwabudu mwengine yeyote.

2- Izungumzie malipo ya wapwekeshaji na adhabu ya washirikina huko Aakhirah pamoja na kuwanusuru wapwekeshaji na kuadhibiwa kwa washirikina duniani.

3- Iamrishe utiifu na kukataza maasi, mambo ambayo ni haki za Tawhiyd na mambo yenye kuikamilisha.

4- Iamrishe kuwa na mapenzi kwa wapwekeshaji na kuwa na chuki kwa washirikina, mambo ambayo yanapelekea katika Tawhiyd.

5- Itoe khabari kuhusu Allaah, majina Yake na sifa Zake, mambo ambayo yanapelekea kumpenda, kumwogopa na kutaraji yale yaliyoko Kwake. Qur-aan tukufu yote ni Tawhiyd, kama alivosema ´Allaamah Ibn-ul-Qayyim.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: I´aanat-ul-Mustafiyd bi Sharh Kitaab-it-Tawhiyd, uk. 15
  • Imechapishwa: 10/09/2019