08. Ni ipi hukumu ya kuzimia wakati wa kufunga?

Swali 08: Ni ipi hukumu ya kuzimia wakati wa kufunga?

Jibu: Kuzimia kumegawanyika sehemu mbili:

1- Ikiwa kuzimia ni kwa siku moja, nusu siku au mfano wa hayo. Kuzimia huku kuna hukumu moja kama kulala.

2- Ikiwa kuzimia ni kwa muda mrefu kama mwezi mmoja au miwili[1]. Mtu kama huyu ana hukumu moja kama mwendawazimu ambaye kalamu imenyanyuliwa kwake.

[1] Koma.

  • Mhusika: ´Allaamah Ahmad bin Yahyaa an-Najmiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaas-Swiyaam, uk. 23-24
  • Imechapishwa: 12/06/2017