08. Ni ipi hukumu ya kupangusa juu ya soksi zilizo na picha ya mnyama?

Swali 08: Ni ipi hukumu ya kupangusa juu ya soksi zilizo na picha ya mnyama?

Jibu: Haijuzu kufuta juu yake. Kupangusa juu ya soksi ni ruhusa na ruhusa haiwi halali kwa madhambi. Maoni yanayosema kuwa inafaa kupangusa juu ya kitu ambacho ni haramu yanapelekea kukubali dhambi hiyo. Ni lazima kukemea kitu cha haramu. Haitakikani kusema kuwa soksi hizo zinatwezwa na kwa ajili hiyo itafaa kupangusa juu yake. Inahusiana na mavazi na kuvaa picha zilizo na mapicha ni haramu kwa hali zote. Kama kwenye soksi kuna picha kwa mfano za simba basi haitofaa kupangusa juu yake.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Buhuuth wa Fataawaa fiyl-Mas´h ´alaal-Khuffayn, katika Majmuu´-ul-Fataawaa (11/165)
  • Imechapishwa: 05/05/2021