Ee Muislamu – Allaah aniwafikishe mimi na wewe katika yale anayoyapenda na kuyaridhia – tambua ya kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliulizwa na Jibriyl (´alayhis-Swalaatu was-Salaam) kuhusu imani ambapo akawa amejibu kwa kusema:

“Imani ni kumwamini Allaah, Malaika Wake, Vitabu Vyake, Mitume Wake, siku ya Mwisho na kuamini Qadar; kheri na shari yake.” Jibriyl (´alayhis-Swalaatu was-Salaam) akamwambia: “Umesema kweli.”

  • Mhusika: ´Allaamah Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab al-Wasswaabiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Qawl al-Mufiyd fiy Adillat-it-Tawhiyd
  • Imechapishwa: 05/08/2020