08. Mtazamo wa Murji-ah al-Fuqahaa´ kwa mtenda dhambi

Murji-ah al-Fuqahaa´ wanaenda kinyume na Aayah na Hadiyth hizi. Lakini pamoja na hivyo kuna tofauti kati ya wao na wale Murji-ah waliopindukia. Murji-ah al-Fuqahaa´ wanaonelea kuwa kuna khatari ya mtenda madhambi kuadhibiwa na kwamba baadhi yao wataingia Motoni. Katika nukta hii wanakubaliana na Ahl-us-Sunnah. Kwa hakika msiba wao ni msiba kweli, lakini mtu anatakiwa kuwa mwadilifu na awe na inswafu na kuelezea tofauti kubwa iliyoko kati ya wao na Murji-ah waliopundikia. Imani imejengwa juu ya uadilifu na inswafu. Hata kafiri haijuzu kumdhulumu. Hali kadhalika mtu wa Bid´ah.

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Qurrat-ul-´Aynayn bi Tawdhwiyh Ma´aaniy ´Aqiydat-ir-Raaziyayn, uk. 18
  • Imechapishwa: 09/10/2016