Suala la kwanza: Sababu zinazojuzisha kutofunga Ramadhaan

Inafaa kutofunga Ramadhaan kwa moja ya nyudhuru zifuatazo:

1- Ugonjwa na utuuzima. Inafaa kwa mgonjwa ambaye anatarajia kupona kula. Atapopona basi ni lazima kwake kulipa zile siku alizoacha kufunga. Amesema (Ta´ala):

أَيَّامًا مَّعْدُودَاتٍ ۚ فَمَن كَانَ مِنكُم مَّرِيضًا أَوْ عَلَىٰ سَفَرٍ فَعِدَّةٌ مِّنْ أَيَّامٍ أُخَرَ

“[Kufunga ni] siku za kuhesabika. Basi atakayekuwa mgonjwa miongoni mwenu au yuko safarini, hivyo basi akamilishe idadi katika siku nyinginezo.”[1]

فَمَن كَانَ مِنكُم مَّرِيضًا أَوْ عَلَىٰ سَفَرٍ فَعِدَّةٌ مِّنْ أَيَّامٍ أُخَرَ

“Basi atakayekuwa mgonjwa miongoni mwenu au yuko safarini, hivyo basi akamilishe idadi katika siku nyinginezo.”[2]

Maradhi ambayo yanamruhusu kuacha kufunga ni yale maradhi ambayo yanamtia uzito  mgonjwa kufunga kwa sababu yake.

Kuhusiana na maradhi ambayo hayatarajiwi kupona au asiyeweza kufunga ushindwaji wa kuendelea, kama mfano wa mtumzima, basi inafaa kwake kula na wala si lazima kwake kulipa. Kitachomlazimu ni yeye kulisha kwa kutoa chakula kumpa maskini kwa kila siku moja iliyompita. Kwa sababu Allaah amefanya kutoa chakula kunalingana na kufunga wakati ambapo mtu alikuwa na chaguo kufanya mawili hayo mwanzoni ambapo kulifaradhishwa funga. Kwa hiyo ndio kitu cha lazima kinachochukua nafasi yake wakati wa udhuru. Imaam al-Bukhaariy (Rahimahu Allaah) amesema:

“Mtumzima asipoweza kufunga, Anas alitoa kulisha chakula baada ya kuwa mtumzima kwa mwaka mmoja au miaka miwili kwa kila siku moja kumlisha maskini. Ibn ´Abbaas amesema kuhusu baba mtumzima na mwanamke mtumzima wasioweza kufunga, wanatakiwa badala yake kumlisha maskini kwa kila siku moja.”[3]

Mtu asiyeweza kufunga kushindwa kusikotarajiwa kuondoka – kwa maradhi au utuuzima – kwa kila siku moja kumlisha maskini nusu pishi ya ngano, tende, mchele au mfano wa hivo katika chakula kilichozoeleka katika mji. Kiwango cha pishi moja ni takriban 2,25 kg. Kwa hiyo atalisha kwa kila siku moja takriban 1125 g.

Haya pamoja na kwamba mgonjwa akifunga funga yake itasihi na kutosheleza.

[1] 02:184-185

[2] 02:184

[3] al-Bukhaariy (4505).

  • Mhusika: Nukhbatin minal-´Ulamaa´
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fiqh-ul-Muyassar, uk. 154-155
  • Imechapishwa: 16/04/2020