Madhambi yananyima utiifu. Lau mtenda dhambi asingelikuwa na adhabu nyingine zaidi ya kwamba anasitishwa na utiifu, basi ingelimtosheleza kutoifanya. Dhambi inasitisha vilevile utiifu wa pili, utiifu wa tatu, utiifu wa nne na kadhalika. Kwa njia hiyo dhambi inasitisha matendo mema mengi. Kila tendo jema katika hayo ni bora kwa mtu kuliko dunia na vile vilivyomo ndani yake. Hili ni kama mfano wa mtu anayekula kitu kinachomsababishia maradhi ya muda mrefu yanayomzuia kula vyakula vilivyo vitamu zaidi kuliko kile cha kwanza.

  • Mhusika: Imaam Ibn Qayyim-il-Jawziyyah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ad-Daa’ wad-Dawaa’, uk. 67
  • Imechapishwa: 05/01/2018