08. Kuritadi kwa kitendo


3- Kukufuru kwa kitendo. Kwa mfano mtu akachinja kwa ajili ya asiyekuwa Allaah. Mtu akichinja kwa ajili ya asiyekuwa Allaah anatoka katika dini na kuritadi kutoka katika sini ya Uislamu. Kwa kuwa amemuabudu asiyekuwa Allaah. Kuchinja ni ´ibaadah. Akichinja kwa ajili ya kitu anachokiadhimisha, vile mfano wa sanamu, kaburi na vyenginevyo katika waungu wa washirikina wa hii leo. Akichinja, ijapokuwa hatotamka, anaritadi. Akichinja au akalisujudia kaburi anakuwa mshirikina. Haijalishi kitu hata kama anaswali, anafunga, anahiji na anasoma Qur-aan. Hakika kaitengua dini yake kwa kitendo hichi cha kishirki.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Nawaaqidh-il-Islaam, uk. 23-24
  • Imechapishwa: 03/05/2018