Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:

Dalili ya jua na mwezi ni maneno Yake (Ta´ala):

وَمِنْ آيَاتِهِ اللَّيْلُ وَالنَّهَارُ وَالشَّمْسُ وَالْقَمَرُ ۚ لَا تَسْجُدُوا لِلشَّمْسِ وَلَا لِلْقَمَرِ وَاسْجُدُوا لِلَّـهِ الَّذِي خَلَقَهُنَّ إِن كُنتُمْ إِيَّاهُ تَعْبُدُونَ

“Na katika ishara Zake ni usiku na mchana na jua na mwezi. Hivyo basi, msisujudie jua na wala mwezi, bali msujudieni Allaah ambaye aliyeviumba [hivyo] ikiwa Yeye pekee mnawambudu.” (41:37)

MAELEZO

Ni dalili yenye kuonyesha kuwa kuna watu wenye kusujudia jua na mwezi. Kwa ajili hii ndio maana Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amekataza kuswali pindi jua linapochomoza na kuzama kwa ajili ya kufunga njia, kwa sababu kuna ambao wanalisujudia jua linapochomoza na linapozama. Kwa hivyo tumekatazwa kuswali katika nyakati hizi mbili hata kama swalah itakuwa kwa ajili ya Allaah. Muda wa kuwa kuswali katika nyakati hizi mbili kunakumbushia kitendo cha washirikina, basi ikakatazwa kwa ajili ya kufunga njia zote zinazopelekea katika shirki. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amekuja kukataza shirki na kukataza vilevile njia zote zinazopelekea kwayo[1].

[1] Tazama “Fath-ul-Majiyd li Sharh Kitaab-it-Tawhiyd (02/835-839).

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh al-Qawaa´id al-Arba´ah, uk. 24-25
  • Imechapishwa: 18/08/2022