Swali: Huku kwetu Suudan anapofariki mtu baada ya siku arobaini familia nzima wanalitembelea kaburi wanawake kwa watoto ambapo wanalifungua kaburi na wanakuwa na nafaka za mahindi na wanazitawanya kwa maiti na naamini pia kuwa humrushia yule maiti changarawe. Je, inafaa kwao kuyatembelea makaburi?

Jibu: Hii ni Bid´ah isiyokuwa na msingi katika Shari´ah. Kurusha mbegu, manukato na nguo yote ni maovu na hayana msingi. Kaburi halifunguliwi isipokuwa wakati wa haja. Kwa mfano ikiwa wafanyakazi wamesahau zana zao, kama vile kipawa, ambapo wakalifungua kwa sababu hiyo, mmoja wao akadondokwa na kitu chenye umuhimu na hivyo wakalifungua kwa sababu hiyo. Ama kulifungua kwa sababu ya mbegu, nguo na mfano wa hayo ni jambo lisilojuzu.

Isitoshe haijuzu kwa wanawake kuyatembelea makaburi. Kwa sababu Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amewalaani wanawake wenye kuyatembelea makaburi. Hayo yamepokelewa kutoka kwa Abu Hurayrah, Ibn ´Abbaas na Hassaan bin Thaabit (Radhiya Allaahu ´anhum). Kwa hivyo haijuzu kwao kuyatembelea. Lakini ni jambo lililowekwa katika Shari´ah kwa wanamme. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Yatembeleeni makaburi. Kwani hakika yanakukumbusheni Aakhirah.”[1]

Ameipokea Muslim katika “as-Swahiyh” yake.

Hekima ya wanawake kukatazwa – na Allaah ndiye mjuzi zaidi – ni kwamba ni mtihani ni wachache wa subira.

[1] Muslim (976).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Tahdhiyr min Fitnat-il-Qubuur, uk. 38-39
  • Imechapishwa: 12/04/2022