08. Kufufuliwa kwa watoto


Miongoni mwa misingi ya imani yenye kumuokoa mtu na kufuru ni kuamini:

1- Kufufuliwa.

2- Malipo.

3- Hesabu.

4- Pepo.

5- Moto. Yote haya ni haki. Allaah (Ta´ala) amesema:

مِنْهَا خَلَقْنَاكُمْ وَفِيهَا نُعِيدُكُمْ وَمِنْهَا نُخْرِجُكُمْ تَارَةً أُخْرَىٰ

“Kutoka humo [ardhini] Tumekuumbeni na katika hiyo [ardhi] Tutakurudisheni na kutoka humo Tutakutoeni mara nyingine.”[1]

وَإِن تَعْجَبْ فَعَجَبٌ قَوْلُهُمْ أَإِذَا كُنَّا تُرَابًا أَإِنَّا لَفِي خَلْقٍ جَدِيدٍ ۗ أُولَـٰئِكَ الَّذِينَ كَفَرُوا بِرَبِّهِمْ ۖ وَأُولَـٰئِكَ الْأَغْلَالُ فِي أَعْنَاقِهِمْ ۖ وَأُولَـٰئِكَ أَصْحَابُ النَّارِ ۖ هُمْ فِيهَا خَالِدُونَ

“Na ukistaajabu basi cha ajabu ni maneno yao: “Je, sisi tukiwa mchanga, hivi kweli [tutafufuliwa] katika umbo jipya?” Hao ni wale waliomkanusha Mola wao. Hao watafungwa minyororo katika shingo zao. Na hao ndio watu wa Motoni, wao humo ni wenye kudumu.”[2]

Katika Aayah kuna dalili yenye kuonesha kuwa yule mwenye kupinga juu ya kufufuliwa amekufuru na kwamba atadumishwa Motoni milele. Allaah atukinge na kufuru na matendo ya kikafiri.

[1] 20:55

[2] 13:05

  • Mhusika: Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ta´liym-us-Swibyaan at-Tawhiyd, uk. 25-27
  • Imechapishwa: 25/03/2017