Ndugu wapendwa! Kufika kwa Ramadhaan ni neema kubwa kwa yule iliyemfikia na akaitendea haki yake kwa kurejea kwa Mola Wake kwa kujiepusha na kumuasi na akamtii, kwa kutokupumbaa na akamtaja na kwa kutokujiweka mbali Naye na akamrejelea:

Ee ambaye dhambi hazikukutosheleza katika Rajab

mpaka akamuasi Mola Wake katika Sha´baan

Hakika umefunikwa na mwezi wa funga baada yake

hivyo usiufanye pia kuwa ni mwezi wa kuasi

Soma Qur-aan na utukuzwe kwayo hali ya kujitahidi

kwani ni mwezi wa kusabihi na Qur-aan

Ni wangapi ulikuwa unawajua miongoni mwa waliofunga hapo kitambo

kuanzia kwa jamaa, majirani na ndugu?

Kifo kimewamaliza na wakakuacha wewe baada yao

ukiwa hai – ni ukaribu ulioje wa aliye mbali kuliko aliye karibu?

Ee Allaah! Tunakuomba utuamshe kutoka katika upumbaaji, utuwafikishe kujifanyia akiba ya kukucha kabla ya kufa, uturuzuku kuchuma wakati wa kipindi cha kumalizika wakati, utusamehe sisi, wazazi wetu na waislamu wote kwa huruma Yako.

Swalah na salamu zimwendee Mtume wetu Muhammad, kizazi chake na Maswahabah zake.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majaalis Shahr Ramadhwaan, uk. 11-12
  • Imechapishwa: 07/04/2020