Kuhusu kuamini siku ya Mwisho kunaingia kuamini yale yote yatayotokea baada ya kufa aliyoelezea Allaah na Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Mfano wa mambo hayo ni kama fitina ya adhabu ya kaburi na neema zake. Vilevile na yale yatayokuwa siku ya Qiyaamah katika hali nzito, njia, mizani, hesabu, malipo, kutawanya madaftari kati ya watu; kuko ambao watapokea madaftari yao kwa mkono wa kulia na wengine watapokea madaftari yao kwa mkono wa kushoto au nyuma ya migongo yao. Kunaingia vilevile kuamini hodhi iliyothibiti ya Mtume wetu Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), Pepo na Moto, waumini kumuona Mola Wao (Subhaanah), kwamba atawazungumzisha na mengineyo yaliyotajwa katika Qur-aan tukufu na Sunnah Swahiyh kutoka kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Ni wajibu kuyaamini na kuyasadikisha yote hayo kwa njia aliyoibainisha Allaah na Mtume Wake.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-´Aqiydah as-Swahiyhah wa maa yudhwaadduhaa, uk. 09
  • Imechapishwa: 30/05/2023