Makadirio kama tulivyotangulia kusema ni siri iliyofichikana ambayo kamwe huwezi kuifichukua. Hivi sasa umesimama kwenye njia mbili. Njia ya kwanza inakuelekeza katika usalama, kufuzu, furaha na heshima. Njia nyingine inayokuelekeza katika maangamivu, majuto na utwevu. Wewe hivi sasa umesimama kati ya njia hizo mbili. Ni mwenye khiyari. Hakuna anayekuzuia kuchukua njia ya upande wa kulia na wala hakuna anayekuzuia kuchukua njia ya upande wa kushoto. Ukitaka, utachukua njia ya kwanza, na ukitaka utachukua njia ya pili. Kusemwe nini lau utachukua njia ya upande wa kulia na kusema kuwa ni makadirio?

Ikiwa utasafiri kwenda katika mji na unaweza kuchagua njia ambayo ni rahisi, fupi na yenye usalama na nyingine sio rahisi, ndefu na haina usalama, tutaona namna utavyochagua ile njia ya kwanza. Hutochukua njia ambayo sio rahisi, ndefu na haina usalama. Haya inahusiana na njia yenye kuhisiwa. Njia ya kimaana ni hali kadhalika. Hakuna tofauti kati ya hayo mawili. Mambo yanahusiana na matamanio ambayo wakati mwingine yanaiongoza na kuishinda akili. Muumini akili yake inatakiwa kuwa yenye kushinda matamanio yake. Endapo ataiacha akili yake timamu iongoze, basi itamfanya aone yale yenye kumdhuru na yenye kumnufaisha na kumfurahisha.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Qadhwaa’ wal-Qadar, katika Majmuu´-ul-Fataawaa (5/221-222)
  • Imechapishwa: 25/10/2016