08. Inafaa kwa mwanamke mjamzito na mwenye kunyonyesha kuacha kufunga?

Swali 08: Inafaa kwa mwanamke mjamzito na mwenye kunyonyesha kuacha kufunga? Je, ni lazima kwao kulipa au kuna kafara juu ya kuacha kwao kufunga?

Jibu: Mwanamke mjamzito na mwenye kunyonyesha swawm ikiwa ngumu kwao basi ni jambo limewekwa katika Shari´ah kwa wao kula. Hata hivyo ni lazima kulipa pindi watapoweza kufanya hivo kama mfano wa mgonjwa. Wapo wanachuoni wenye kuonelea kwamba inatosha kwao kulisha masikini kwa kila siku moja walioacha kufunga. Lakini hata ni maoni dhaifu yaliyoshindwa nguvu. Maoni ya sawa ni kwamba ni lazima kwao kulipa kama anavofanya msafiri na mgonjwa. Allaah (´Azza wa Jall) amesema:

فَمَن كَانَ مِنكُم مَّرِيضًا أَوْ عَلَىٰ سَفَرٍ فَعِدَّةٌ مِّنْ أَيَّامٍ أُخَرَ

“Basi atakayekuwa mgonjwa miongoni mwenu au yuko safarini, hivyo basi akamilishe idadi katika siku nyinginezo.” (02:184)

Kumefahamisha juu ya hayo Hadiyth ya Anas bin Maalik al-Ka´biy aliyesimulia ya kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Allaah amemwondoshea msafiri funga na nusu ya swalah na mjamzito na mnyonyeshaji swawm.”

Wameipokea wale watano.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdllaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: As-ilah Muhimmah tata´alaqah bisw-Swiyaam, uk. 17-18
  • Imechapishwa: 12/04/2019