08. Hadiyth “Yule mwenye kusema ´hapana mwabudiwa wa haki isipokuwa Allaah` na akafa… “

985- Hudhayfah (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza:

“Nilimvuta Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kifuani mwangu ambapo akasema: “Yule mwenye kusema ´hapana mwabudiwa wa haki isipokuwa Allaah` na akafa, ataingia Peponi. Mwenye kufunga siku moja kwa ajili ya Allaah na akafa, ataingia Peponi. Mwenye kutoa swadaqah kwa ajili ya Allaah na akafa, ataingia Peponi.”[1]

Ameipokea Ahmad kwa cheni ya wapokezi isiyokuwa na neno. al-Aswbahaaniy ameipokea vilevile kwa tamko lisemalo:

“Ee Hudhayfah! Mwenye kufunga siku moja kwa ajili ya Allaah (´Azza wa Jall) kisha akafa, basi Allaah atamwingiza Peponi.”[2]

[1] Swahiyh.

[2] Swahiyh kupitia zengine.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Adhwiym bin ´Abdil-Qawiy al-Mundhiriy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb (01/579)
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy