08. Hadiyth “Ukitaka funga na ukitaka kula”


Mlango unaozungumzia kufunga safarini

Hadiyth ya kwanza

1- ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anhaa) amesimulia: “Hamzah bin ´Amr al-Aslamiy – alikuwa ni mtu anayefunga sana – alimwambia Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam): “Je, nifunge nikiwa safarini?” Akajibu: “Ukitaka funga na ukitaka kula.”

Maana ya kijumla:

Maswahabah (Radhiya Allaahu ´anhum) walitambua kwamba Shari´ah yenye huruma haikuwaruhusu kula safarini isipokuwa ni kwa sababu ya kuwaonea huruma. Hamzah al-Aslamiy alikuwa ni mtu mwenye nguvu juu ya kufunga na alikuwa ni mtu anayependa kheri. Alikuwa ni mtu anayependa kufunga sana Allaah amuwie radhi. Ndipo akamuuliza Mtume wa Allaah  (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam): “Nifunge nikiwa safarini?” Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akampa khiyari kati ya kufunga na kula na akamwambia: “Ukitaka funga na ukitaka kula.”

Faida zinazochukuliwa kutoka katika Hadiyth:

1- Ruhusa ya kuacha kufunga safarini. Kwa sababu safari ina uzito.

2- Khiyari ya kufunga na kutokufunga kwa yule ambaye ana nguvu ya kufunga. Tunakusudia swawm ya Ramadhaan…

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdullaah bin ´Abdir-Rahmaan al-Bassaam
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Taysiyr-ul-´Allaam Sharh ´Umdat-il-Ahkaam, uk. (01/325-326)
  • Imechapishwa: 04/06/2018