731- Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Pengine mmoja wenu anasubiri achukue zizi la kondoo na kwenda nao mbali masafa ya maili moja au maili mbili ambapo akakosa chakula ikambidi asogee mbele na swalah ya ijumaa ikamfikia na asende na wala asiishuhudie [na swalah ya ijumaa nyingine ije ambapo na wala asiishuhudie na ije swalah ya ijumaa nyingine na asiishuhudie][1] mpaka kupigwe muhuri kwenye moyo wake?”[2]

[1] Ziada iko kwa Ibn Maajah na Ibn Khuzaymah na inatiliwa nguvu na Hadiyth inayofuatia.

[2] Nzuri kupitia zengine.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb (1/452)
  • Imechapishwa: 02/05/2020
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy