Haafidhw Ibn Hajar al-´Asqalaaniy (Rahimahu Allaah) amesema:

687- ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anhaa) amesema:

“Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akipaka wanja ilihali amefunga katika Ramadhaan.”[1]

Ameipokea Ibn Maajah kwa cheni ya wapokezi nyonge. at-Tirmidhiy amesema:

“Hakukusihi kitu juu ya maudhui haya.”

MAELEZO

Inafaa kwa mfungaji kupaka wanja na kutia machoni dawa za matone ya maji? Ndio, inafaa kwa mujibu wa maoni sahihi. Kwa sababu msingi ni uhalali mpaka kuwepo dalili inayokataza. Hata kama Hadiyth ya ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anhaa) iliyotajwa ni dhaifu sisi hatuihitajii kwa sababu msingi ni uhalali mpaka kuwepo dalili inayokataza. Wala hakujapokelewa kitu kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwamba amekataza kupaka wanja wakati wa funga. Kujengea juu ya haya mfungaji anayo ruhusa ya kupaka wanja, atie dawa ya matone ya maji machoni na dawa ya matone ya maji masikioni. Hakuna neno hata kama tutakadiria kuwa atahisi ladha ya dawa hii kooni, kwa sababu mambo haya sio kula wala kunywa isipokuwa ni kujitibu. Jengine ni kwamba sio dawa inayoingizwa kupitia sehemu ya kawaida. Macho na masikio sio njia za kawaida kama pua. Mtu akiweka dawa ya matone ya maji puani na yakafika tumboni mwake anafungua. Lakini machoni hapana kwa sababu sio njia ya kawaida.

[1] Ibn Maajah (1678).

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ash-Sharh al-Mukhtaswar ´alaa Buluugh-il-Maraam (2/414-417)
  • Imechapishwa: 24/04/2020