74- Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza kwamba amemsikia Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akisema:

”Dunia ni yenye kulaaniwa[1]. Kila kilichomo ndani yake ni chenye kulaaniwa isipokuwa kumdhukuru Allaah, yote Anayoyapenda, mwanachuoni na yule mwenye kujifunza.”[2]

Ameipokea at-Tirmidhiy, Ibn Maajah na al-Bayhaqiy. at-Tirmidhiy amesema:

“Hadiyth ni nzuri.”

[1] Makusudio ni kila kile chenye kumshughulisha na kumuweka mtu mbali na Allaah (Ta´ala). Kusema kwamba ni yenye kulaaniwa bi maana ni yenye kutengwa mbali na uangalizi Wake.

[2] Nzuri.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Adhwiym bin ´Abdil-Qawiy al-Mundhiriy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb (1/141)
  • Imechapishwa: 15/09/2018
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy