08. Hadiyth “Alikuwa amefungua vifungo… “

45- ´Urwah bin ´Abdillaah bin Qushayr amesema: Mu´aawiyah bin Qurrah amenihadithia, kutoka kwa baba yake ambaye amesema:

“Nilimwendea Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akiwa na kikundi cha wanamme kutoka Muzaynah. Tukampa kiapo cha usikivu na utiifu. Alikuwa amefungua vifungo ambao nikaingiza mkono wangu kwenye mfuko wa kanzu yake ambapo nikagusa muhuri.” ´Urwah amesema: “Sikupatapo kamwe kumuona Mu´aawiyah wala mtoto wake wakifunga vifungo, sawa wakati wa majira ya baridi au majira ya joto.”[1]

Ameipokea Ibn Maajah na Ibn Hibbaan katika ”as-Swahiyh” na tamko ni lake.

[1] Swahiyh.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Adhwiym bin ´Abdil-Qawiy al-Mundhiriy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb (1/126)
  • Imechapishwa: 26/04/2020
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy