08. Fadhila ya ´ibaadah za usiku


Amesema Allaah (Ta´ala):

يَا أَيُّهَا الْمُزَّمِّلُ قُمِ اللَّيْلَ إِلَّا قَلِيلًا نِصْفَهُ أَوِ انقُصْ مِنْهُ قَلِيلًا أَوْ زِدْ عَلَيْهِ وَرَتِّلِ الْقُرْآنَ تَرْتِيلًا إِنَّا سَنُلْقِي عَلَيْكَ قَوْلًا ثَقِيلًا

”Ee uliyejifunika. Simama (kuswali) usiku kucha isipokuwa (muda) mdogo tu. Nusu yake, au ipunguze kidogo. Au izidishe, na soma Qur-aan kwa Tartiyl (ipasavyo kwa polepole na sauti nzuri). Hakika Sisi Tutaweka juu yako kauli nzito.” (al-Muzammil 73 : 01-05)

وَمِنَ اللَّيْلِ فَتَهَجَّدْ بِهِ نَافِلَةً لَّكَ عَسَىٰ أَن يَبْعَثَكَ رَبُّكَ مَقَامًا مَّحْمُودًا

”Na katika usiku, amka ufanye ‘ibaadah nayo (Qur-aan katika Swalaah ya Tahajjud) ninaafilah (Sunnah ziada) kwako. Huenda Mola wako Akakuinua cheo kinachosifika.” (al-Israa´ 17 : 79)

وَمِنَ اللَّيْلِ فَاسْجُدْ لَهُ وَسَبِّحْهُ لَيْلًا طَوِيلًا

”Na katika usiku, msujudie na mtakase usiku (muda) mrefu.” (ad-Dahr 76 : 26)

41- Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Mola Wetu Hushuka kila usiku katika mbingu ya dunia pindi kunapobaki theluthi ya usiku ya mwisho na Anasema: “Ni nani mwenye kuniomba nimuitikie? Ni nani mwenye kuniomba nimpe? Ni nani mwenye kuniomba msamaha nimsamehe?”

42- Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Mja anakuwa karibu zaidi na Mola Wake theluthi ya mwisho ya usiku. Ukiweza kuwa miongoni mwa wanaomdhukuru Allaah katika wakati kama huo, basi fanya hivyo.”

43- Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Hakika usiku kuna saa ambayo hakuna Muislamu yeyote anayemuomba Allaah (´Azza wa Jalla) kheri katika mambo ya dunia au Aakhirah isipokuwa Anampa nacho. Hilo huwa katika kila usiku:

وَالْمُسْتَغْفِرِينَ بِالْأَسْحَارِ

“Na watoaji na waombao maghfirah kabla ya Alfajiri.” (Aal ´Imraan 03 : 17)

  • Mhusika: Shaykh-ul-Islaam Ahmad bin Taymiyyah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ul-Kalim at-Twayyib, uk. 42-44
  • Imechapishwa: 21/03/2017