08. Dalili juu ya mguu wa Allaah 8

8 na 9 – Muhammad bin Makhlad ametuhadithia: Muhammad bin Ishaaq as-Swaaghaaniy ametuhadithia: Hasan al-Ashyab ametuhadithia: Hammaad bin Salamah ametuhadithia, kutoka kwa Yuunus, kutoka kwa ´Ubayd, kutoka kwa Ayyuub as-Sikhtiyaaniy na Habiyb ash-Shahiyd, kutoka kwa Abu Hurayrah, kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliyesema:

“Pepo na Moto vilizozana ambapo Moto ukasema: “Ndani yangu wanaingia wakandamizaji, wafalme na watukufu.” Pepo nayo ikasema: “Ndani yangu wanaingia watu mafukara na masikini.” Ndipo Akasema kuuambia Moto: “Wewe ni adhabu Yangu ambayo namsibu yule Ninayemtaka.” Akasema kuiambia Pepo: “Wewe ni huruma Yangu inayokienea kila kitu. Kila mmoja wenu atajazwa.” Kuhusu Moto kutatupwa ndani yake na utasema:

هَلْ مِن مَّزِيدٍ

“Hakuna zaidi?”[1]

mara tatu mpaka pale (Tabaarak wa Ta´ala) Atapoweka unyayo Wake juu yake. Hapo ndipo utajikusanya na kusema: “Tosha, tosha.”

Katika upokezi wa Abu Hurayrah imekuja ya kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alisema:

“Tosha, tosha.”

[1] 50:30

  • Mhusika: Imaam ´Aliy bin ´Umar ad-Daaraqutwniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kitaab-us-Swifaat, uk. 43-44
  • Imechapishwa: 22/10/2017