08. Asiyeichukua dini kwa Maswahabah amepotea na ni mzushi


Imaam al-Barbahaariy (Rahimahu Allaah) amesema:

Yule asiyechukua kutoka kwao amepotea na kuzusha. Kila Bid´ah ni upotevu na upotevu na watu wake ni Motoni.

Bi maana asiyechukua dini yake kutoka kwao hayuko kaitka haki. Kwa sababu wao ndio walionukuu Qur-aan na Sunnah. Wakitukanywa ina maana nukuu zao zinabatilika. Haya ndio makusudio ya maadui wa Allaah na Mtume Wake. Makusudio yao ni kuuharibu Uislamu lakini hata hivyo wameonelea waje na hila hizi chafu ili waweze kukata mafungamano kati ya waliokuja nyuma na waislam waliotangulia. Malengo ni kuwepo wepesi wa kuwajaribu wale waliokuja nyuma. Endapo watafungamana na al-Jamaa´ah ya awali na wakafungamana na Qur-aan na Sunnah kutakuwa hakuna wepesi. Bali watashindwa kwa idhini ya Allaah.

Yule asiyechukua kutoka kwao atakuwa amepotea katika haki na kuzusha.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Sharh-is-Sunnah, uk. 19
  • Imechapishwa: 11/10/2017