17- Akishafariki na roho ikakatika kwenda kwa Mola Wake, basi yanawalazimu mambo yafuatayo:

1 na 2 – Wanatakiwa kumfumba macho yake na vilevile kumuombea du´aa. Hayo ni kutokana ya Umm Salamah aliyesimulia:

“Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliingia kwa Abu Salamah ilihali macho yake yamemtoka ambapo akamfumba kisha akasema: “Roho inapochukuliwa  inasindikizwa na macho. Watu wakapiga makelele katika watu wake. Akasema: “Msijiombe dhidi ya nafsi zenu isipokuwa kwa kheri. Kwani Malaika huitikia “Aamiyn” kwa yale mnayoyasema.” Kisha akasema:

اللهم اغفر لأبي سلمة، وارفع درجته في المهديين، واخلفه في عقبه في الغابرين، واغفر لنا وله يا رب العالمين، وافسح له في قبره، ونور له فيه

 “Ee Allaah! Msamehe Abu Salamah, ipandishe daraja yake katika wale waliotangulia, mkaimu kwa kizazi chake katika wale aliowaacha, msamehe yeye na sis, ee Mola wa walimwengu, mpanulie ndani ya kaburi lake na umtilie nuru ndani yake.”

 Ameipokea Muslim na Ahmad (06/297), al-Bayhaqiy (03/334) na wengineo.

3- Wamfunike kwa nguo inayositiri mwili mzima. Hayo ni kutokana na Hadiyth ya ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anhaa) aliyesimulia kwamba:

“Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) pindi alipofariki alifunikwa kwa shuka ya kiyemeni yenye misitarimisitari.”

Ameipokea al-Bukhaariy na Muslim katika “as-Swahiyh zao”, al-Bayhaqiy (03/385) na wengineo.

4- Haya ni juu ya yule ambaye amekufa hali ya kuwa si Muhrim. Kwani Muhrim hafunikwi kichwa chake wala uso wake. Hayo ni kutokana na Hadiyth ya Ibn ´Abbaas (Radhiya Allaahu ´anhumaa) aliyesimulia:

“Wakati bwana mmoja alipokuwa amesimama katika viwanja vya ´Arafah tahamaki akaanguka kutoka juu ya mnyama wake ambapo akamkanyaga shingoni” au alisema “akamuua papo hapo.” Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akasema:

“Muosheni kwa maji yaliyochanganyikana na mkunazi na mumkafini katika nguo zake mbili.”

Katika upokezi mwingine imekuja:

“Katika nguo zake.”

msimpake mafuta ya maiti.

Katika upokezi mwingine imekuja:

“Wala msimtie manukato.”

wala msimfunike kichwa chake (wala uso wake). Kwani hakika atafufuliwa siku ya Qiyaamah akiwa ni mwenye kuleta Talbiyah.”

Ameipokea al-Bukhaariy na Muslim katika “as-Swahiyh zao”, Abu Na´iym katika “al-Mustakhraj” (q. 139-140) na al-Bayhaqiy (03/390) na ziada haiko katika al-Bukhaariy.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ahkaam-ul-Janaa-iz wa Bid´ahaa, 22-23
  • Imechapishwa: 19/12/2019