07. Uondoshwaji wa neno “bin” kati ya jina la baba na mtoto ni jambo limetoka Ulaya

Nitataja uhakika wa kihistoria muhimu. Neno “bin” kati ya jina la baba na mtoto ni jambo lililokuwepo kwa tabaka zote za watu. Wakati ambapo Ulaya ilianza mambo ya kuwachukua watoto wadogo na kuwafanya wa kwao ndipo watu wakatofautisha kati ya mtoto wa damu na yule wa aliyefanywa kuwa ni mtoto wao kwa neno “bin”. Ikawa inasemwa kwa yule mwana wa damu “fulani bin fulani” na yule aliyechukuliwa ikawa inasemwa “fulani fulani”. Ndipo “bin” ikapotea katika majina yote. Baadaye “bin” ikapotea hata katika miji ya waislamu mnamo karne 1900. Ndipo watu wakawa wanasema kwa mfano “Muhammad ´Abdullaah”. Huu ni usulubu uliozuliwa na uliotoka nje usiojulikana na waarabu na kiarabu.

Uliwahi kusikia mtu akisema kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) anaitwa Muhammad ´Abdullaah? Lau mtu angesema hivyo basi angelitiwa adabu. Ni kwa nini tusimuige Mtume ambaye ndiye mwongozaji na mwadilifu bora kabisa wa njia?

Tazama jinsi utolewaji wa neno “bin” ulivyosababisha utatizi inapokuja katika jina lenye ushirikiano kati ya jinsia zote mbili kama mfano wa Asmaa´ na Khaarijah. Kwenye karatasi mtu hawezi kujua kama majina haya ni ya mwanaume au mwanamke isipokuwa kwa kuwepo neno “bin” na “bint.”

  • Mhusika: ´Allaamah Bakr bin ´Abdillaah Abu Zayd
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Tasmiyat-ul-Mawluwd, uk. 07
  • Imechapishwa: 18/03/2017