07. Ni sharti kunuia kupangusa na muda wa kupangusa?


Swali 6: Ni wajibu kupangusa juu ya khufuu mtu anuie upangusaji na kama anapangusa kama mkazi au msafiri?

Jibu: Katika hali hii nia sio wajibu. Hukumu ya kitendo imehusishwa na kupatikana kwake na hivyo hakuna haja ya kunuia. Vivyo hivyo inahusiana na mtu anaevaa nguo; sio sharti anuie kufunika sehemu zake za siri [´Awrah] wakati anaposwali. Kadhalika haishurutishwi katika kuvaa khufuu mtu akanuia kupangusa juu yake. Hata muda vilevile. Ikiwa ni msafiri ana michana mitatu na nyusiku zake sawa ikiwa atanuia au hatonuia na mkazi ana mchana mmoja na usiku wake sawa ikiwa atanuia au hatonuia.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Buhuuth wa Fataawaa fiyl-Mas´h ´alaal-Khuffayn, katika Majmuu´-ul-Fataawaa (11/165)
  • Imechapishwa: 04/05/2021