07. Mtume Muhammad kwa watoto


Swali 6: Ni nani Mtume wako?

Jibu: Mtume wetu ni Muhammad bin ´Abdillaah bin ´Abdil-Muttwalib bin Haashim bin ´Abdil-Manaaf.

Allaah (Ta´ala) amemteua kutoka kwa Quraysh. Quraysh ndio kabila bora kutoka katika kizazi cha Ismaa´iyl. Allaah amemtuma Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwa watu weupe na weusi. Allaah amemteremshia Kitabu na hekima. Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akawalingania watu katika kumuabudu Allaah peke yake na kuacha vyenginevyo walivyokuwa wakiviabudu badala ya Allaah katika masanamu, miti, manabii, watu wema, malaika na vyenginevyo.

Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akawalingania watu katika kujiepusha na shirki. Akawapiga vita ili waache shirki na badala yake wamuabudu Allaah peke yake. Allaah (Ta´ala) amesema:

قُلْ إِنَّمَا أَدْعُو رَبِّي وَلَا أُشْرِكُ بِهِ أَحَدًا

“Sema: “Hakika mimi namuomba Mola wangu Pekee na wala simshirikishi na yeyote.”[1]

قُلِ اللَّـهَ أَعْبُدُ مُخْلِصًا لَّهُ دِينِي

“Sema: “Allaah Pekee namwambudu nikimtakasia Dini yangu kwa ajili Yake.”[2]

قُلْ إِنَّمَا أُمِرْتُ أَنْ أَعْبُدَ اللَّـهَ وَلَا أُشْرِكَ بِهِ ۚ إِلَيْهِ أَدْعُو وَإِلَيْهِ مَآبِ

“Sema: “Hakika mimi nimeamrishwa nimwabudu Allaah na nisimshirikishe na chochote. Kwake nalingania na Kwake ni marejeo yangu.”[3]

قُلْ أَفَغَيْرَ اللَّـهِ تَأْمُرُونِّي أَعْبُدُ أَيُّهَا الْجَاهِلُونَ وَلَقَدْ أُوحِيَ إِلَيْكَ وَإِلَى الَّذِينَ مِن قَبْلِكَ لَئِنْ أَشْرَكْتَ لَيَحْبَطَنَّ عَمَلُكَ وَلَتَكُونَنَّ مِنَ الْخَاسِرِينَ بَلِ اللَّـهَ فَاعْبُدْ وَكُن مِّنَ الشَّاكِرِينَ

“Sema: “Je, mnaniamrisha nimuabudu asiyekuwa Allaah enyi majahili?” Kwa yakini umefunuliwa Wahy na kwa wale walio kabla yako kwamba: Ukifanya shirki bila shaka zitaporomoka ‘amali zako na bila shaka [Aakhirah] utakuwa miongoni mwa waliokhasirika. Bali Allaah Pekee mwabudu na uwe miongoni mwa wenye kushukuru.”[4]

[1] 72:20

[2] 39:14

[3] 13:36

[4] 39:64-66

  • Mhusika: Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ta´liym-us-Swibyaan at-Tawhiyd, uk. 22-25
  • Imechapishwa: 25/03/2017