07. Msimamo wa Salaf juu ya sifa

19- Yahyaa bin ´Ammaar amesema katika kijitabu chake baada ya kutaja idadi kubwa ya maimamu wa Ahl-ul-Hadiyth katika Maswahabah na waliokuja baada yao:

“Hakuna yeyote katika sisi, sawa wale waliotangulia na waliokuja nyuma, ambaye amejiakhirisha kuzungumza juu ya sifa, kukifasiri Kitabu cha Allaah (´Azza wa Jall) au kuyafasiri maneno ya Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), kuzidisha kitu katika Qur-aan na Sunnah au kupunguza kitu ndani yavyo. Hatuvuki mipaka, hatufananizi na wala hatuzidishi juu ya yale yaliyomo katika Qur-aan na Sunnah.

20- Imaam Abu Bakr Muhammad bin Khuzaymah amesema:

“Khabari kuhusu sifa ni zenye kuafikiana na Qur-aan. Karne zilizokuja nyuma walinukuu kutoka karne zilizotangulia, kutoka kwa Maswahabah mpaka wakati wetu huu, kwa njia ya kwamba ni sifa za Allaah (Ta´ala). Mtu anatakiwa kumjua, kumuamini na kujisalimisha kwa yale aliyoeleza Allaah (Ta´ala) katika uteremsho Wake na yale Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliyosema kuhusu Kitabu Chake. Mtu afanye hivo pasi na kupindisha maana wala kukanusha, na kuacha kufananiza na kufanya namna.

21- Abu Bakr ´Abdullaah bin Muhammad bin Ahmad ametukhabarisha: Abu Bakr at-Twuraythiythiy ametuhadithia: Abul-Qaasim Hibatullaah ametuhadithia: Muhammad bin Ahmad bin ´Ubayd ametuhadithia: Muhammad bin al-Hasan ametuhadithia: Ahmad bin Zuhayr ametuhadithia: ´Abdul-Wahhaab bin Najdah al-Huutiy ametuhadithia: Baqiyyah ametuhadithia: al-Awzaa´iy ametuhadithia

“az-Zuhriy na Mak-uul walikuwa wakisema: “Zipitisheni Hadiyth hizi kama zilivyokuja.”

  • Mhusika: Imaam Muwaffaq-ud-Diyn bin Qudaamah al-Maqdisiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Dhamm-ut-Ta’wiyl, uk. 16
  • Imechapishwa: 02/06/2018