Allaah (Ta´ala) amesema:

فَمَن كَانَ مِنكُم مَّرِيضًا أَوْ عَلَىٰ سَفَرٍ فَعِدَّةٌ مِّنْ أَيَّامٍ أُخَرَ

“Yule atakayekuwa mgonjwa miongoni mwenu au safarini, basi akamilishe idadi [ya siku zilizompita] katika siku nyinginezo.”[1]

Inajuzu kwa mgonjwa kuacha kufunga na kulipa masiku mengine. Nia yake inatakiwa iwe kulipa masiku hayo pale ambapo Allaah (´Azza wa Jall) atapomponya.

Inajuzu vilevile kwa msafiri kuacha kufunga iwapo atanuia kuyalipa masiku yake pindi aaporejea nyumbani.

Maradhi ambayo yanaruhusu kuacha kufunga yanatofautiana. Mgonjwa ambaye ni mgonjwa sana kwa kiasi kwamba hawezi kufunga hata mara moja hatakiwi kufunga, kwa kuwa anajidhuru.

Iwapo maradhi yatakuwa mepesi kwa kiasi cha kwamba mgonjwa anaweza kufunga lakini pamoja na uzito, huyu inafaa kwake kufunga lakini hata hivyo imechukizwa. Lakini atatakiwa asifunge endapo ataonelea kuwa inamtaabisha.

Ikiwa daktari mmoja au wawili wa kiislamu watahakikisha kuwa swawm inamzidishia maradhi, itakuwa ni wajibu kwake kuacha kufunga.

Je, lililo bora kwa yule mgonjwa ambaye anaweza kufunga pamoja na kupata uzito mdogo afunge au aache kufunga? Lililo bora kwake ni yeye kufunga.

Swali hilo hilo limeulizwa juu ya msafiri. Lililo bora kwa msafiri ni yeye kufunga au kuacha kufunga? Wanachuoni wametofautiana juu ya hili. Kuna ambao wamependekeza afunge. Wengine wamependekeza asifunge. Lakini hata hivyo tofauti hii inahusiana na pale ambapo kutakuwa hakuna tabu katika kufunga. Ikiwa kutapatikana uzito hakuna tofauti kwamba bora ni kuacha kufunga.

[1] 02:184

  • Mhusika: ´Allaamah Ahmad bin Yahyaa an-Najmiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Tafsiyr Aayaat-is-Swiyaam, uk. 12-14
  • Imechapishwa: 02/06/2017