Shaykh Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimhu Allaah) amesema:

Msingi wa pili:

Allaah ameamrisha kuwa na umoja katika dini na akakataza kufarikiana kwayo. Allaah amebainisha haya ubainifu wenye kutosheleza ambao unafahamika na wajinga. Ametukataza kuwa kama wale waliotofautiana na wakafarikiana kabla yetu na wakaangamia na akataja kuwa amewaamrisha waislamu kuwa na umoja katika dini na kuwakataza kufarikiana katika hiyo dini. Linazidisha hilo uwazi zaidi kwa yale yaliyokuja katika Sunnah – ni katika ajabu ya maajabu katika hayo.

Halafu jambo la kutofautiana katika misingi na matawi ikawa ndio elimu na uelewa katika dini. Mambo yakawa amri ya kuwa na umoja katika dini hasemi jambo hilo isipokuwa zindiki au mwendawazimu.

MAELEZO

Allaah ameamrisha… – Msingi wa pili miongoni mwa misingi iliyotajwa na Shaykh (Rahimahu Allaah):

“Kuwa na umoja katika dini na makatazo ya kufarikiana kwayo.”

Msingi huu mtukufu umejulishwa na Qur-aan, Sunnah, matendo ya Maswahabah (Radhiya Allaahu ´anhum) na Salaf (Rahimahumu Allaah).

Kuhusu Qur-aan Allaah (Ta´ala) amesema:

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اتَّقُوا اللَّـهَ حَقَّ تُقَاتِهِ وَلَا تَمُوتُنَّ إِلَّا وَأَنتُم مُّسْلِمُونَ  وَاعْتَصِمُوا بِحَبْلِ اللَّـهِ جَمِيعًا وَلَا تَفَرَّقُوا ۚ وَاذْكُرُوا نِعْمَتَ اللَّـهِ عَلَيْكُمْ إِذْ كُنتُمْ أَعْدَاءً فَأَلَّفَ بَيْنَ قُلُوبِكُمْ فَأَصْبَحْتُم بِنِعْمَتِهِ إِخْوَانًا وَكُنتُمْ عَلَىٰ شَفَا حُفْرَةٍ مِّنَ النَّارِ فَأَنقَذَكُم مِّنْهَا ۗ كَذَٰلِكَ يُبَيِّنُ اللَّـهُ لَكُمْ آيَاتِهِ لَعَلَّكُمْ تَهْتَدُونَ

“Enyi walioamini! Mcheni Allaah ukweli wa kumcha na wala msife isipokuwa nyinyi ni waislamu na shikamaneni kwa kamba ya Allaah nyote pamoja wala msifarikiane na kumbukeni neema ya Allaah juu yenu, pale mlipokuwa maadui, kisha akaunganisha nyoyo zenu, mkawa kwa neema Yake ndugu na [ilihali hapo kabla] mlikuwa ukingoni mwa shimo la Moto hivyo akakuokoeni kutoka ndani yake – hivyo ndivyo Allaah anakubainishieni Aayah Zake mpate kuongoka.”[1]

وَلَا تَكُونُوا كَالَّذِينَ تَفَرَّقُوا وَاخْتَلَفُوا مِن بَعْدِ مَا جَاءَهُمُ الْبَيِّنَاتُ ۚ وَأُولَـٰئِكَ لَهُمْ عَذَابٌ عَظِيمٌ

“Na wala msiwe kama wale waliofarikiana na wakakhitilafiana baada ya kuwajia hoja ya wazi – na hao watapata adhabu kuu.”[2]

وَلَا تَنَازَعُوا فَتَفْشَلُوا وَتَذْهَبَ رِيحُكُمْ

“Na wala msizozane, mtavunjikwa moyo na zikatoweka nguvu zenu.”[3]

إِنَّ الَّذِينَ فَرَّقُوا دِينَهُمْ وَكَانُوا شِيَعًا لَّسْتَ مِنْهُمْ فِي شَيْءٍ

“Hakika wale waliofarakisha dini yao na wakawa makundimakundi, huna lolote kuhusiana na wao.”[4]

شَرَعَ لَكُم مِّنَ الدِّينِ مَا وَصَّىٰ بِهِ نُوحًا وَالَّذِي أَوْحَيْنَا إِلَيْكَ وَمَا وَصَّيْنَا بِهِ إِبْرَاهِيمَ وَمُوسَىٰ وَعِيسَىٰ ۖ أَنْ أَقِيمُوا الدِّينَ وَلَا تَتَفَرَّقُوا فِيهِ

“Amekuwekeeni Shari´ah katika dini yale aliyomuusia kwayo Nuuh, na ambayo tumekufunulia Wahy na tuliyomuusia kwayo Ibraahiym na Muusa na ‘Iysaa kwamba simamisheni dini na wala msifarikiane humo.”[5]

Katika Aayah hizi Allaah amekataza kufarikiana na akabainisha mwisho wake mbaya kwa mtu mmojamoja, jamii na taifa zima.

[1] 03:102-103

[2] 03:105

[3] 08:46

[4] 06:159

[5] 42:13

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Usuwl-is-Sittah, uk. 13-14
  • Imechapishwa: 17/06/2021