07. Lengo la Allaah kuwatumiliza Mitume

… na akamfanya kutokuwa na udhuru kupitia kwa Mitume ambao ndio viumbe bora kabisa –  Allaah hakumwacha mtu huyu aitegemee elimu yake mwenyewe na ile akili aliyompa. Alimtumia Mitume ili wapate kumbainishia ni namna gani anatakiwa kumwabudu Mola wake na anatakiwa kuchukua msimamo gani kwa mujibu wa Shari´ah (´Azza wa Jall). Mitume ni neema kutoka kwa Allaah (´Azz wa Jall). Mtu hawezi kufanya lolote pasi na Mitume. Hata kama ni mwenye mapenzi juu ya kheri si mwenye kuweza. Kwa ajili hiyo ndio maana Allaah (´Azza wa Jall) akamtumilizia Mitume na akamteremshia Vitabu. Makusudio ni ili wambainishie namna gani anatakiwa kumwabudu Mola wake. Hii ni miongoni mwa rehema za Allaah (´Azza wa Jall) na kumtilia Kwake umuhimu mwanadamu huyu:

رُّسُلًا مُّبَشِّرِينَ وَمُنذِرِينَ لِئَلَّا يَكُونَ لِلنَّاسِ عَلَى اللَّـهِ حُجَّةٌ بَعْدَ الرُّسُلِ

“Mitume ni wabashiriaji na waonyaji ili pasikuweko kutoka kwa watu hoja yoyote juu ya Allaah baada ya kuletwa Mitume hao.”[1]

Viumbe bora zaidi ni Mitume (Swalla Allaahu ´alayhim wa sallam).

[1] 04:165

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Bayaan-ul-Ma´aaniy fiy Sharh Muqaddimati Ibn Abiy Zayd al-Qayrawaaniy, uk. 14
  • Imechapishwa: 01/07/2021