07. Kuvaa cheni, uzi na mfano wavyo kwa ajili ya kuondosha au kuzuia dhara ni shirki

1- Allaah (Ta´ala) amesema:

قُلْ أَفَرَأَيْتُم مَّا تَدْعُونَ مِن دُونِ اللَّـهِ إِنْ أَرَادَنِيَ اللَّـهُ بِضُرٍّ هَلْ هُنَّ كَاشِفَاتُ ضُرِّهِ

”Sema: “Je, mnaonaje wale mnaowaomba badala ya Allaah ikiwa Allaah atanitakia dhara, je, wao wataweza kuondosha dhara Yake?” (39:38)

2- ´Imraan bin Husayn (Radhiya Allaahu ´anh) amesimulia kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alimuona mtu mkononi mwake kavaa kicheni [cha mfano wa pete] ya shaba. Akamuuliza: “Ni kitu gani hichi?” Mtu yule akajibu: “Kinanikinga na udhaifu.”´Akasema: “Kivue. Kwani hakika hakikuzidishii isipokuwa udhaifu. Lau ungekufa nawe bado wakivaa usingelifaulu kamwe.”

Ameipokea Ahmad kwa mlolongo wa wapokezi usiokuwa na neno. Amepokea vilevile kupitia kwa ´Uqbah bin ´Aamir (Radhiya Allaahu ´anh) kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

3- “Yeyote atakayevaa hirizi, basi Allaah hatomtimizia na yule atakayevaa au kutundika chaza ndogo, Allaah asimpe raha yoyote.”[1]

Katika upokezi mwingine imekuja:

4- “Yeyote atakayevaa hirizi ameshirikisha.”[2]

5- Ibn Abiy Haatim amepokea kutoka kwa Hudhayfah (Radhiya Allaahu ´anh) alimuona mtu ambaye mkononi mwake kulikuwa kipande cha uzi anataka umponye homa. Akaukata ule uzi na akasoma maneno Yake:

وَمَا يُؤْمِنُ أَكْثَرُهُم بِاللَّـهِ إِلَّا وَهُم مُّشْرِكُونَ

”Wengi kati yao hawamwamini Allaah isipokuwa wao ni wenye kufanya shirki.” (12:106)

MAELEZO

Mlango huu haukusomwa kwa Imaam Ibn Baaz (Rahimahu Allaah).

[1] Ahmad (17440), Abu Ya´laa (1759) na at-Twahaawiy (6660). Nzuri kwa mujibu wa Shu´ayb al-Arnaa’uut katika ”Musnad-ul-Imaam Ahmad”.

[2] Ahmad (17458). Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy katika ”Swahiyh-ul-Jaami´” (11340).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Kitaab-it-Tawhiyd, uk. 38
  • Imechapishwa: 23/06/2018