Swali 07: Nikimtembelea mgonjwa asiyeweza kuswali msikitini nyumbani kwake na ukafika wakati wa swalah nikiwa nyumbani kwake ambapo akaniomba kumtolea swadaqah kwa kuswali pamoja nao na nisende kuswali msikitini. Je, inafaa kwangu kufanya hivo[1]?

Jibu: Ni lazima kwako kuswali pamoja na mkusanyiko. Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Yeyote atakayesikia adhaana na asiitikie basi hana swalah isipokuwa akiwa na udhuru.”[2]

Ibn ´Abbaas (Radhiya Allaahu ´anh) aliulizwa ni nini udhuru ambapo akasema: “Khofu au maradhi.”

Kuhusu mgonjwa ni mwenye kupewa udhuru kuswali nyumbani kwake. Anapata fadhilah za swalah ya mkusanyiko kwa sababu ya udhuru. Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Akigonjweka mja au akasafiri, basi huandikiwa mfano wa yale aliyokuwa akiyafanya akiwa mkazi na mzima.”[3]

Ameipokea al-Bukhaariy katika “as-Swahiyh” yake.

[1] Majmuu´-ul-Fataawaa (12/53-54)

[2] Ibn Maajah (785).

[3] al-Bukhaariy (2996).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ahkaam Swalaat-il-Jumu´ah wal-Jamaa´ah, uk. 32-33
  • Imechapishwa: 25/11/2021