12- Kwa wale ambao Miyqaat yao ni Dhul- Hulayfah basi imependezwa kwao kuswali hapo. Swalah hii sio kwa sababu ya umaalum wa Ihraam, bali ni kwa sababu ya sifa maalum ya mahali na baraka. al-Bukhaariy amepokea kutoka kwa ´Umar (Radhiya Allaahu ´anh) akisimulia kwamba amemsikia Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akisema kwenye bonde la ´Aqiyq:

“Wakati wa usiku amenijia mimi mwenye kuja kutoka kwa Mola wangu na akasema: “Swali katika bonde hili lenye kubarikiwa na akasema: “´Umrah – na katika upokezi mwingine “´Umrah na hajj.””

Ibn ´Umar ameeleza kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliyesema:

“Alionekana na hali ya kuwa ni mwenye kuteremka wakati wa usiku kwa ajili ya kupumzika hapo Dhul-Hulayfah katikati ya bonde. Akaambiwa: “Hakika wewe uko katika Batwhaa´ lililobarikiwa.””[1]

[1] Tazama “Swahiyh Abiy Daawuud” (1579) na “Mukhtaswar Swahiyh Muslim” (761-762) – Allaah asahilishe chapisho lake. Haafidhw amesema:

“Katika Hadiyth tunapata kufahamu kwmaba fadhilah za ´Aqiyq ni kama fadhilah za al-Madiynah na fadhilah za kuswali hapo… ” (Fath-ul-Baariy (3/311))

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Manaasik-ul-Hajj wal-´Umrah, uk. 16
  • Imechapishwa: 06/07/2018