Lengo la saba: Kushuhudia manufaa makubwa ya hajj

Miongoni mwa malengo makubwa ya hajj ni kushuhudia manufaa makubwa ya hajj, mawaidha yenye kuathiri na darsa mbalimbali. Allaah (Ta´ala) amesema:

وَأَذِّن فِي النَّاسِ بِالْحَجِّ يَأْتُوكَ رِجَالًا وَعَلَىٰ كُلِّ ضَامِرٍ يَأْتِينَ مِن كُلِّ فَجٍّ عَمِيقٍ لِّيَشْهَدُوا مَنَافِعَ لَهُمْ

“Tangaza kwa watu hajj watakufikia kwa kutembea kwa miguu na juu ya kila ngamia aliyekonda watakuja kutoka katika kila njia pana za milima zilioko mbali kabisa. Ili wapate kushuhudia manufaa yao.”[1]

Manufaa na faida za hajj hayawezi kudhibitiwa. Mazingatio na masomo yake hayawezi kudhibitiwa na kuhesabiwa. Maneno Yake (Ta´ala):

لِّيَشْهَدُوا مَنَافِعَ لَهُمْ

“Ili wapate kushuhudia manufaa yao.”

yanaonyesha kuwa ni mengi na yamekusanya manufaa aina mbalimbali. Kushuhudia manufaa haya ni jambo lenye kulengwa katika hajj. Kwa sababu “Laam” iliokuja katika maneno Yake:

لِّيَشْهَدُوا مَنَافِعَ لَهُمْ

“Ili wapate kushuhudia manufaa yao.”

ni “Laam” yenye kuonyesha sababu. Imefungamana na maneno Yake:

وَأَذِّن فِي النَّاسِ بِالْحَجِّ يَأْتُوكَ رِجَالًا وَعَلَىٰ كُلِّ ضَامِرٍ

“Tangaza kwa watu hajj watakufikia kwa kutembea kwa miguu na juu ya kila ngamia aliyekonda… “

Bi maana ukiwatangazia kuhiji basi watakujia hali ya kutembea kwa miguu na wengine wakiwa wamepanda vipando kwa ajili ya kushuhudia na wajionee wenyewe manufaa ya hajj. Makusudio ya kujionea wenyewe ni wayapate na wanufaike kwayo.

Kujengea juu ya haya inatakiwa kwa wale wote waliowafikishwa na Allaah (´Azza wa Jall) juu ya neema hii na wakasahilishiwa kutekeleza ´ibaadah hii wawe ni wenye pupa kwelikweli ya kupata manufaa ya hajj, kunufaika na mawaidha na mazingatio yake. Ukiongezea juu ya ule ujira na thawabu nyingi atazopata, kusamehewa madhambi, kufutiwa makosa. Ni zaidi kwa yule mwenye kupata faida hii na akafuzu kwa ngawira hii arudi katika nchi yake akiwa na hali takasifu, nafsi safi na maisha mapya yaliyojawa na imani na kumcha Allaah hali ya kuwa ni mwenye kuamrisha mema, mazuri, msimamo katika dini na kuhifadhi kumtii Allaah (´Azza wa Jall).

[1] 22:27-28

  • Mhusika: Shaykh ´Abdur-Razzaaq bin ´Abdil-Muhsin al-´Abbaad
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Maqaaswid-ul-Hajj, uk. 35-37
  • Imechapishwa: 18/08/2018