07. Kuoga josho kubwa baada ya kuchomoza kwa alfajiri

Swali 7: Akitwahirika mwenye hedhi au mwenye damu ya uzazi kabla ya alfajiri na asiwahi kuoga isipokuwa baada ya alfajiri swawm yake inasihi?

Jibu: Ndio, funga ya mwanamke mwenye hedhi inasihi akitwahirika kabla ya alfajiri na asiwahi kuoga isipokuwa baada ya kuchomoza kwa alfajiri. Vivyo hivyo mwenye damu ya uzazi. Kwa sababu kipinid hicho wamekuwa miongoni mwa watu wanaotakiwa kufunga. Wanawake hawa ni wenye kufanana na ambaye yuko na janaba. Ikichomoza alfajiri ilihali yuko na janaba basi swawm yake inasihi. Amesema (Ta´ala):

فَالْآنَ بَاشِرُوهُنَّ وَابْتَغُوا مَا كَتَبَ اللَّـهُ لَكُمْ ۚ وَكُلُوا وَاشْرَبُوا حَتَّىٰ يَتَبَيَّنَ لَكُمُ الْخَيْطُ الْأَبْيَضُ مِنَ الْخَيْطِ الْأَسْوَدِ مِنَ الْفَجْرِ

“Basi sasa changanyikeni nao [waingilieni] na tafuteni Aliyokuandikieni Allaah kwenu. Kuleni na kunyweni mpaka ubainike kwenu weupe wa alfajiri katika weusi wa usiku.”[1]

Allaah akiidhinisha jimaa mpaka pale kutapobainika alfajiri basi itapelekea kuoga kufanyike baada ya kuchomoza kwa alfajiri. Isitoshe ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anhaa) amesimulia kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akiamka akiwa na janaba linalotokana na mke wake ilihali amefunga. Kwa msemo mwingine yeye (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa anaoga baada ya kuchomoza kwa alfajiri.

[1] 02:187

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: 60 su-aal wa jawaab fiy Ahkaam-il-Haydhw, uk. 11-12
  • Imechapishwa: 13/06/2021